December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yataifisha madini ya mamilioni

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam imetaifa madini yenye gramu zaidi ya 800 ya mfanyabiashara Haji Hassan (52) na Jamas Hassan (55). Anaripoti Faki Sosi  …(endelea).

Kutaifishwa kwa madini hayo yenye thamani zaidi ya Sh. Mil 500, ni ni sehemu ya hukumu kwa wafanyabiashara hao walihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini sh. Mil 1, baada ya kutiwa hatia kwa makosa ya kufanya biashara ya madini kinyume cha sheria,

Hukumu hiyo imetolewa leo tarehe 23 Disemba 2020, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya baada ya watuhumiwa hao kukiri makosa yao.

Watuhumiwa hao walishtakiwa kwenye mahakama hiyo kwa makosa ya kuhujumu uchumi pamoja na kufanya biashara ya madini bila kuwa na kibali.

Watu hao walikamatwa wakifanya shughuli hiyo Mtaa wa Lumumba na Uhuru, Kariakoo jijiji Dar es Salaam mapema mwaka huu.

Awali, watuhumiwa hao waliandikia barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kukiri makosa yao na kuomba kufunguliwa pazia la makubaliano.

Katika mazungumzo hayo, walitakiwa kulipa Sh. Mil 40  kama fidia ya makosa hayo ambayo tayari iliishalipwa.

Hakimu Mfawidhi Isaya amesema, madini hayo  yatataifashwa na kwamba, yatakuwa mali ya serikali ambapo mahakama hiyo imemkabidhi Wakili Mwandimizi wa serikali ili akayakabidhi kwenye mamlaka husika.

Watuhumiwa hao wamelipa faini na wameachiwa huru.

error: Content is protected !!