Mahakama kuu nchini Kenya imeruhusu jeshi la nchi hiyo KDF kutumiwa katika kuwasaidia polisi kupambana na maandamano ya kupiga mswada wa fedha. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Hata hivyo, serikali imepewa siku mbili kutoa mwongozo wa kipindi na sehemu ambako jeshi litatumika katika kurejesha hali ya utulivu baada ya maandamano ya Jumanne na jana Alhamisi.
Katika uamuzi wake siku ya jana Alhamisi, Jaji Lawrence Mugambi alisema wanajeshi wamefunzwa kutumia nguvu, sio kutangamana na raia.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi iliyowasilishwa na Chama cha Mawakili nchini Kenya (LSA), Jaji aliuliza maswali kadhaa kwa pande zote zilizokuwepo huku akitaka kuelewa vipengele vya operesheni za kijeshi na sheria mahususi kwa vikosi vya ulinzi.
Aliitaka LSK kutoa maoni kuhusu matukio ambayo KDF inaweza kutumwa ambapo chama hicho ilitaja kifungu cha 241 cha katiba.
Kwa upande wake, serikali inatetea hatua yake ikisema hakuna chochote kinachokiuka sheria katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa na Waziri wa Ulinzi Aden Duale.
Leave a comment