WAKULIMA na wafugaji wametakiwa kutokichagua tena Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025, kwa madai kuwa Serikali yake imeshindwa kuwaondolewa tozo na ushuru wa kinyonyaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo umetolewa leo tarehe 4 Juni 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.
“Ukandamizaji ni mfumo pacha wa unyonyaji, nchi hii sio wakulima na wafugaji pekee ni watumishi wote mpaka hawa askari wanaotulinda nso wananyonywa. Serikali wanakusanya majela mengi lakini huduma mbovu,” amesema Lissu.
Lissu amesema “Tanzania hii kuna shida kila mahali na zote zinatokana na watawala wenu hiyo ni dharau ya CCM kwenu wananchi mwaka huu na 2025 wote tuamue kusema tumechoka kunyonywa.”
Leave a comment