Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Lema: Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lema: Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa

Spread the love

MJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa aliyekuwa kada mwenzake wa cha hicho, Mchungaji Peter Msigwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).


Lema ambaye pia alikuwa Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa Chadema kanda ya kaskazini, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, amesema amesikitika kwa sababu alidhani wangeendelea kuwa timu moja na kufanya kazi ya siasa kwa masilahi ya umma.

“Hata hivyo, namtakia kila la heri huko alikoenda maana kila mtu ana ndoto katika maisha yake na angependa zitimie,” amesema Lema.

Msigwa ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa ,leo tarehe 30 Juni amejiunga CCM na kupokewa na Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hiko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msigwa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona  Chadema kimepoteza uhalali wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia  kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania.

Pia baada ya kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na Chadema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Rais Samia kugharamia matibabu ya kijana aliyetekwa

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan amesema yeye binafsi atabeba gharama zote...

Habari za SiasaKimataifa

Waandamanaji wasambaza majeneza Nairobi

Spread the loveWAKATI vijana wa Kenya wakitekeleza kile walichomuahidi Rais wa taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Yakubu awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Comoro

Spread the loveBalozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu, leo Jumanne amewasilisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Kobe Motor Japan kuongeza idadi ya magari yake soko la Tanzania

Spread the loveKampuni ya Kobe Motor ya Japan imesema itaendelea kujitanua zaidi...

error: Content is protected !!