Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Korea yatoa bilioni 422 ujenzi hospitali Binguni
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Korea yatoa bilioni 422 ujenzi hospitali Binguni

Screenshot
Spread the love

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Korea zimesaini Mkataba wa Mkopo nafuu wa Sh  422.16 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni, Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkataba wa Mkopo huo umesainiwa jijini Soeul leo tarehe 5 Juni 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Natu Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa Korea umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya Exim – Korea, Hwang Kiyeon.

Mkopo huo ni moja ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Korea iliyoanza tarehe 31 Mei 2024.

Screenshot

Ujenzi wa Hospitali hiyo utahusisha majengo ya Hospitali yenye vitengo vinne vya magonjwa Maalum kama ya kina mama na watoto, Kituo cha Mafunzo, nyumba za makazi kwa wafanyakazi, ununuzi na ufungaji wa vifaa vya matibabu vya teknolojia ya kisasa na usimikaji wa mfumo wa afya wa mawasiliano.

Screenshot

Uwekaji saini wa mkataba huo umeshuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Zanzibar, Dk. Saada Mkuya ambaye alieleza kuwa ujenzi huo utakapokamilika utaongeza upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa watu wa Zanzibar.

Pia amesema utapunguza idadi ya vifo kutokana na kuimarika kwa huduma bora za afya na matumizi ya vifaa vya kisasa na utahamasisha utoaji wa mafunzo bora ya elimu ya afya kutokana na ujenzi wa Kituo cha Mafumzo kitakachokuwa na vifaa vya kisasa vya kujifunzia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!