Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamati yamkuta Mpina na hatia, yapendekeza afungiwe vikao 10
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kamati yamkuta Mpina na hatia, yapendekeza afungiwe vikao 10

Spread the love

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kupitia kwa Mwenyekiti wake, Ally Juma Makoa imemkuta na hatia Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina (CCM) kwa kueleza kuwa “amedharau mamlaka ya Spika na mwenendo wa Shughuli za Bunge”. Anaripoti Mwandishi Wetu (endelea.)

Kamati hiyo imependekeza Bunge linaazimie Mpina apewe adhabu kwa mujibu wa kifungu cha 84 (3a) cha kanuni za Bunge toleo 2023 ya kutohudhuria vikao vya bunge 10 mfululizo kuanzia leo tarehe 24 Juni 2024.

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina

Kamati imeeleza kuwa imejiridhisha kwamba kitendo alichofanya Mpina ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Bunge kwa sababu ya kudharau Mamlaka ya Spika, kuingilia mwenendo wa shughuli za Bunge na vilevile ni kitendo kinachofedhehesha, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Ally Juma Makoa amesema kitendo cha Mpina kuitisha Mkutano wa Waandishi wa Habari na kutoa ufafanuzi wa ushahidi alioupeleka kwa Spika ni kukiuka Kifungu cha 34 (1) (g) vya Sheria ya Kinga, Madaraka na Hadhi ya Bunge, Sura 296 kinachokataza kusambaza kwa umma, Taarifa zinazofanyiwa kazi na Bunge pasipo kupata kibali cha Bunge.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu jioni bungeni jijini Dodoma wakati Mwenyekiti huyo akisoma maoni ya kamati kuhusu ushahidi wa Mpina kuthibitisha tuhuma dhidi ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kusema uongo bungeni na kulipotosha Bunge na

Pia amesoma taarifa ya tuhuma dhidi ya Mpina kudharau mamlaka ya spika, Bunge na mwenendo wa shughuli za Bunge.

“Hivyo, Kamati inaliomba Bunge litafakari shauri hili linalomhusu Luhaga Mpina, ushahidi uliopo, Sheria na Kanuni na kuuzingatia wakati wa kupitisha Azimio la kutoa adhabu anayostahili kwa kosa alilotenda,” amesema.

Akisoma azimio la Bunge, mwenyekiti huyo amesema tarehe 4 Juni mwaka huu Mpina alimtuhumu Bashe kwa kusema uongo na kupotosha Bunge kuhusu suala la upungufu wa sukari.

“Spika alimueleza Mpina kuwasilisha ushahidi tuhuma dhidi ya waziri wa kilimo ifikapo tarehe 14 Juni 2024.

Aliwasilisha ushahidi tarehe 14 kisha kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kufafanua kabla bunge halijafanyia kazi.

“Tarehe 16 Juni kwa mujibu wa kanuni za bunge uliagiza kamati kushughulikia suala la vitendo vya Mpina kutoa ushahidi aliouwasilisha kwako tarehe 14 Juni,” amesema.

Amesema kwa kuwa kamati ilichunguza na kumtia hatiani kwa kukiuka masharti ya 26 (d,e) cha sheria ya kinga, madaraka na hadhi ya bunge sura 296 pamoja na kanuni ya 84 (j,k) kwa kuwasilisha kwenye vyombo vya habari nyaraka aliyowasilisha kwa spika.

“Kitendo ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa bunge na spika kudharau mamlaka ya spika, kuingilia mwenendo wa shughuli za bunge vinaathiri na kuvunja heshima ya bunge mbele ya watanzania.

“Bunge linaazimia Mpina apewe kwa mujibu wa kifungu cha 84 (3a) kanuni za Bunge toleo 2023 kutohudhuria vikao vya bunge 10 mfululizo kuanzia leo tarehe 24 Juni 2024,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Maandamano yaibuka upya Kenya

Spread the loveVIJANA wa Kenya waliojipachika jina la Generation Z (Gen Z)...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CAG atoa kongole kwa PPAA

Spread the loveMDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...

error: Content is protected !!