Sunday , 30 June 2024
Home Kitengo Biashara Kamari kodi juu kwenda kuchangia bima ya afya
BiasharaHabari za SiasaTangulizi

Kamari kodi juu kwenda kuchangia bima ya afya

Vijana waki-bet
Spread the love

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye thamani ya dau la kamari kwenye michezo ya kubahatisha na Bahati Nasibu ya Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema mapato yatakayokusanywa kutoka chanzo hiki ni kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo na makundi maalum hususan wanawake wajawazito na watoto wa umri chini ya miaka mitano.

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025, amesema hatua hiyo inatarajia kupeleka kiasi cha Sh. 29.5 bilioni kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Pia amependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye ada ya matangazo ya biashara za Michezo ya Kubahatisha na Bahati Nasibu ya Taifa yanayotangazwa kupitia vituo vya televisheni, redio, na tasnia ya uchapishaji.

“Lengo la hatua hii ni kuongeza wigo wa kodi. Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 9,150,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Biashara

Cheza sloti za Expanse kasino! mamilioni yanakusubiri 

Spread the love  Leo ni zamu yako kushinda na kuibuka Mfalme wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

error: Content is protected !!