Friday , 28 June 2024
Home Kitengo Biashara IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa
BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the love

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi yake ya utendaji imeidhinisha ufadhili wa dola milioni 786.2 (Sh trilioni 2) kwa Tanzania kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Shirika hilo la kifedha linakamilisha pia tathmini tofauti ya kuruhusu malipo ya dola milioni 149.4 (Sh bilioni 3.8) kwa ajili ya msaada wa bajeti.

Mamlaka za Tanzania zina dhamira ya kuendelea kutekeleza mageuzi ya kudhibiti uthabiti wa kifedha, kuimarisha ufufuaji wa uchumi, kukuza ukuaji endelevu na shirikishi, IMF ilisema katika taarifa.

Katika miaka mitatu iliyopita, utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ulifanya mageuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kurudisha ukuaji wa uchumi katika kiwango cha ukuaji wa pato la taifa la kabla ya janga la Covid wa asilimia 6 hadi asilimia 7.

Mpango wa mageuzi ya uchumi wa Tanzania bado umeendelea kuwa imara, IMF imesema, na kuongeza kuwa ukuaji wa uchumi uliongezeka mwaka 2023 baada ya kupungua mwaka 2022.

Uchumi wa Tanzania ambao unategemea utali, madini, kilimo na viwanda, umeendelea kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa yanayochochewa na kuongezeka kwa sekta ya huduma, kulingana na Benki ya Dunia.

Uchumi wa Tanzania unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka huu, kutoka asilimia 5.1, waziri wa mipango na uwekezaji katika Ofisi ya Rais, Kitila Mkumbo alisema wiki iliyopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the loveRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

Biashara

Expanse kasino inaitika na mamilioni kila siku

Spread the love ISHI KIFALME kwa kucheza Kasino, Meridianbet kunapromosheni kubwa ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watanzania waonywa kutotumia uchaguzi kuvuna hela

Spread the loveWATANZANIA wametakiwa kutotumia uchaguzi kuwa wakati wa mavuno ya pesa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Spread the loveWakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika...

error: Content is protected !!