Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Doyo autaka Uenyekiti wa ADC
Habari za Siasa

Doyo autaka Uenyekiti wa ADC

Spread the love

 

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa, Doyo Doyo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa baada ya Mwenyekiti wa Sasa Hamad Rashid Mohamed kumaliza muda wake kikatiba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia Scola Kahana aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini mwaka 2020 kupitia Chama hicho ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa Ili aweze kushirikiana na Mwenyekiti Taifa kukinoa Chama hicho na kukiwezesha kuwa Chama Cha mfano

Akitangaza nia yake mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema ameona kuwa anatosha kugombea nafasi hiyo na endapo atafanikiwa atapambana Ili kuendelea kukiimarisha kiweze kufikia viwango vya juu

“Kutokana na uzoefu wa miaka 10 nilioupata kutoka kwa Mwenyekiti aliiyemaliza muda wake naahiidi kuyaendeleza mazuri yote hususan kuilinda katiba ya chama.

Alisema Juni 11 mwaka huku atachukua fomu rasmi kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo na kuwaomba wanachama wenzake ndani ya chama itakapofika Juni 27 mwaka huku wamchague Ili aweze kufanya yote aliyokusudia na Chama kiweze kufikia viwango vya juu.

Doyo alimshukuru Mwenyekiti anayemaliza muda wake kwa kuilinda katiba ya chama aliyoitumikia kwa awamu mbili na kukubali kuachia ngazi huo ni mfano mzuri kwa kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa na tabia ya kung”ang”ania madaraka

*Katikà utaratibu huu Hamad Rashid ametufundisha jambo hususan vyama vya Siasa na hili liwe somo kwa viongozi wengine kutoka vyama mbalimbali wakiwemo vizazi vipya,”alisema Doyo.

Aisha aliingeza kusema kuwa endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo atakisaidia Chama kusukuma ajenda za upatikanaji wa ajira,elimu Bora,na kupata wabunge wawakilishi watakaowakilisha wananchi katikà changamoto zao bungeni .

Naye Mwenyekiti wa Vijana Taifa Ibrahimu Pogora alimpongeza Doyo kwa kutangaza Nia yake na kuahidi kushirikiana naye katikà harakati zote za uchaguzi,kupata wadhamini Bara na visiwani

Aliwataka wanachama wa Chama hicho kutambua kuwa wanadhamana na mtia Nia wa nafasi hiyo kwa kuwa Doyo si mwanachama wa kuletwa bali ni mwanzilishi wa Chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!