Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, wamekopa jumla ya Sh 17.2 trilioni kutoka katika vyanzo vya nje kwa lengo la kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Amesema fedha hizo zimeelekezwa kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo: Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa vipande mbalimbali pamoja na ununuzi wa mabehewa na vichwa vya treni.
Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025, amesema mikoa itakayonufaika na mradi huu ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Katavi na Kigoma.
“Miradi hii pia itafungua fursa za kiuchumi kutoka nchi jirani kama vile Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” amesema.
Leave a comment