Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Biteko: 93% ya uvuvi ni wavuvi wadogo
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: 93% ya uvuvi ni wavuvi wadogo

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema asilimia 93 ya uvuvi wote hapa nchini unategemea wavuvi wadogo na hivyo ni lazima uwe endelevu kwa manufaa ya sekta nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wavuvi kufanyika baranı Afrika sambamba na Maadhimisho ya miaka 10 ya mafanikio ya sekta ya uvuvi yanayofanyika hapa nchini, Dk. Biteko amesema, bila uvuvi mdogo hakuna viwanda vya samaki wala hakuna samaki kwenye soko.

Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha bado sekta ya uvuvi mdogo haijafikiwa vya kutosha na hivyo kutoa wito kwa wadau wote kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa wavuvi wadogo na kuwaendeleza kwa manufaa ya sekta hiyo.

Dk. Biteko amesema wavuvi wadogo wakiendelezwa basi wavuvi wakubwa watapatikana na hivyo mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa utakuwa mkubwa.

Ametoa wito kwa wadau wote kuangalia namna ya kuwawezesha wavuvi wadogo kwa nyenzo, mitaji, elimu na kuangalia namna ya kupata soko la bidhaa za wavuvi wadogo barani Afrika.

Aidha, amewataka wadau wa sekta ya uvuvi  barani Afrika  kuhakikisha wanaifanyia kazi sekta ya uvuvi ili kuhakikisha inachangia kwenye pato la Taifa kwa kuhakikisha rasilimalizi za uvuvi zinalindwa.

“Nitoe wito kwenu wadau wa sekta ya uvuvi nchini kuhakikisha mnawapa kipaumbele wavuvi wadogo kwani ndio wanaochangia takribani asilimia 95 ya uvuvi wote Tanzania”, amesema  Dk. Biteko

Ameongeza “Takwimu zinaonesha kuwa nchi Tanzania  inazalisha wastani wa tanı 475,579 za  samaki katı ya hızo tani 429,168 zinatokana na uvuvi katika maji ya asılı na kuchangia kiasi cha shilingi trilioni 3.4 ambapo ni karibu  na asilimia1.9 kwa mwaka”.

Aidha, Dk. Biteko amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa kwenye sekta ya uvuvi Tanzania Kama ilivyo kwa bara la Afrika bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi,ushirikishwaji mdogo wa wadau katika usimamizi wa shughuli za uvuvi hususani wanawake na vijana pamoja na upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa ni heshima kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa kwanza Afrika wa Wavuvi Wadogo ambao chimbulo lake ni Mkutano wa kuadhimisha Mwaka wa Kimataifa wa Wavuvi Wadogo na Wafugaji Viumbe kwenye Maji (IYAFA) uliofanyika Rome nchini Italia Machi, 2023.

Ameongeza kuwq lengo la Mkutano huo wa Kwanza wa Wavuvi Wadogo Afrika ni kutoa fursa kwa Wavuvi Wadogo kushiriki na kupaza sauti zao juu ya kuboresha uvuvi mdogo ikiwa ni pamoja na kuwezesha ushirikishwaji wa wavuvi wadogo kwenye michakato ya uundwaji na utekelezaji wa sera, sheria, kanuni, mipango na mikakati yote inayohusu wavuvi wadogo.

“Ni muhimu kusema kwamba uchaguzi wa Tanzania haukuwa kwa bahati, ila ni kwa kutambua umuhimu wa uvuvi mdogo kwenye nchi yetu, na hatua ambazo nchi imechukua katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Nchi wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa Uvuvi Mdogo”, amesema Ulega.

Amefafanua kuwa Kauli mbiu ya Mkutano huo “Muongo mmoja wa Maendeleo: Kuongelea baadaye ya Uvuvi Mdogo Endelevu“ ilichaguliwa kutokana na kusherekea miaka kumi ya utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa  Uvuvi Mdogo ili kufikia uvuvi mdogo endelevu. Mkutano huu utafanya tathmini ya hali halisi ya utekelezaji Mwongozo huo wa hiyari, sambamba na utekelezaji wa muundo wa kisera na Mkakati wa Mageuzi ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Afrika.

“Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Duniani kuandaa Mpango kazi wa kutekeleza Mwongozo wa Hiyari wa wavuvi wadogo ambapo katika mkutano huu tutapata fursa ya kueleza uzoefu wetu kwa nchi nyingine.” Amesisitiza Ulega.

Waziri wa Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka nchini Malawi, Dk. Michael Bizwick Usi amesema kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama wanapaswa kujadili masuala yanayohusu sekta ya uvuvi mdogo barani Afrika na kuangalia namna bora ya kuboresha kutokana na changamoto zilizopo.

Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Ang’ele Makombo N’tumba amesema kuwa kuna haja ya kuwasaidia wanawake katika sekta ya wavuvi wadogo na kuwa SADC kwa kushirikiana na wadau watasaidia nchi wanachama ili kuboresha sekta hiyo pamoja na kuzuia uvuvi haramu.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Dkt. Tipo Nyabenyi Tito amesema licha ya kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wavuvi wadogo ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na kuwa FAO itashirikiana na wadau wa sekta ya wavuvi wadogo kwa kukuza uelewa na uwezo kwa wavuvi hao.

Kwa upande wake, Rais wa Mtandao wa Wavuvi Wadogo Barani Afrika, Gaoussou Gueye amesema kuwa sekta ya uvuvi mdogo ni muhimu hivyo inatakiwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuongeza tija ya shughuli za uvuvi na kuwa wanawake wako katika sekta mbalimbali kuanzia ukusanyaji wa samaki hadi kuuza kwa walaji.

“Kama tunataka kusaidia uvuvi uwe endelevu lazima tuwe na mazingira wezeshe kwa wanawake ili kuleta usalama wa chakula katika bara la Afrika na utoshelevu wa chakula, katika uchumi wa buluu tunapaswa kulinda uchumi wetu kwa kukuza sekta kwa maendeleo ya Afrika,” amesema Gueye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!