Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Itunda akemea imani potofu zinazosababisha ubakaji
Habari Mchanganyiko

DC Itunda akemea imani potofu zinazosababisha ubakaji

Spread the love

VITENDO vya ubakaji, mauaji yatokanayo na visa vya wivu wa mapenzi na imani za kishirikina, vimetajwa kuwa ni moja ya changanoto zinazoikumba jamii hali inayosababisha kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili. Anaripoti Ibrahim Yassin … Songwe, (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana Jumanne na Mkuu wa wilaya ya Songwe, Solomoni Itunda katika hitimisho la mkutano wa injili uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Ichenjezwa wilayani Mbozi.

Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, Itunda amesema viongozi wa nyumba za Ibada na waumini wengine wana nafasi kubwa kukemea vitendo hivyo wakiwa kwenye mikutano ama madhabahuni ili jamii iishi kwa kumtegemea Mungu.

Mkutano huo ulioendeshwa na uongozi wa kanisa la New Life in Christ ambayo ni muungano wa makanisa mbalimbali ya kikristo nchini, umefanyika kwa muda wa siku saba mkoani Songwe.

Akiwasilisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan, Itunda ameeleza kuwa Rais Samia anatambua  kazi inayofanywa na viongozi wa dini ndiyo maana amekuwa akishirikiana nao katika mambo mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CAG atoa kongole kwa PPAA

Spread the loveMDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...

Habari Mchanganyiko

TRA Morogoro kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara 27

Spread the love MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro inatarajia...

error: Content is protected !!