Sunday , 7 July 2024
Home Kitengo Biashara Bwire Mtendaji mpya DAWASA
BiasharaHabari Mchanganyiko

Bwire Mtendaji mpya DAWASA

Spread the love

Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika leo tarehe 3 Julai, 2024 ofisi za DAWASA Dar Es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano DAWASA imesema Mhandisi Bwire ni Mtumishi wa Wizara ya Maji ambaye amehudumu kama Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Kibaha.

Pia amewahi kuhudumu katika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA).

na hadi anapokea jukumu hilo alikua ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika  Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Bwire amechukua nafari ya Kiunga Kingu ambaye alisimamishwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu uhaba wa maji Dar es Salaam.

Aweso pia alimsimamisha kazi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji-DAWASA, Shaban Mkwanywe na kuiweka DAWASA chini ya uangalizi Wizara ili kuboresha utendaji wake kufuatia uzembe uliopelekea visima kukosa maji na kufanya Wakazi wa Dar es salaam kukosa maji.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mamilioni kwa kucheza kasino na sloti ya Sticky 777

Spread the love  Moja kati ya biashara nzuri na yenye mtaji mdogo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Spread the loveUamuzi wa Serikali ya Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa...

error: Content is protected !!