Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Butiku: Kumchangia fedha Samia kwa ajili ya uchaguzi ni rushwa
Habari za Siasa

Butiku: Kumchangia fedha Samia kwa ajili ya uchaguzi ni rushwa

Spread the love

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation), Mzee  Joseph Butiku, amekemea tabia ya baadhi ya watu kumchangia fedha Rais Samia Suluhu Hassan, kwa  ajili ya  kuchukua fomu ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, akisema ni rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mzee Butiku ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa kongamano la miaka mitatu ya Taasisi ya Kizalendo Tanzania Patriotic Organisation (TPO), jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi CCM kinachanga mnafanya nini hiko? Niwaambie mimi ni mzee mmeanza kumchangia kabla ya uchaguzi wa mwaka kesho wanachanga Leo hiyo ni rushwa tu. Mkitaka leo kuniripoti Mzee Butiku amesema kumchangia Rais ni rushwa mseme,” amesema Mzee Butiku.

Mzee Butiku amesema tabia ya kumchangia wagombea hela itaongeza rushwa kwani ikifika wakati wa chaguzi watu watalazimika kuchanga hela kwa wagombea wanaowahitaji ili waweze kushinda.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema aliwahi kutofautiana na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayatu Benjamin Mkapa kuhusu suala la kutoa rushwa kwa wananchi ili wamchague.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!