Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh 155.4 bilioni zinatarajiwa kupungua kwenye mapato ya Serikali kutokana na pendekezo la kufanya maamuzi ya muda mfupi ya kugharamia malipo ya nyongeza ya mkupuo kwa watumishi wa umma waliostaafu kuanzia mwaka 2022/2023 na watakaostaafu kuendelea hadi 2029/2030. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Amependekeza malipo ya mkupuo kwa wastaafu kwa asilimia saba ili kufikia asilimia 40 kwa kundi ambalo lilikuwa linalipwa asilimia 50 kabla ya kuunganishwa kwa mifuko ya pensheni.
Pia amependekeza kuongeza kikokotoo kwa asilimia mbili ili kufikia asilimia 35 kwa kundi ambalo lilikuwa linalipwa asilimia 25 kabla ya kuunganishwa kwa mifuko ya pensheni.
Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025, amesema nyongeza hizo zitaanza kulipwa kwa wastaafu waliostaafu kuanzia mwaka 2022/23 na kuendelea hadi watakaostaafu mwaka 2029/30 na baada ya hapo mfuko wa PSSSF uchukue jukumu la kuendelea kuwalipa mafao.
“Lengo la hatua hii ni kutoathiri mfumo mzima wa pensheni kwa kuwa na uwiano wa mafao kwa wanachama na kuupa Mfuko muda wa kuangalia uhimilivu wake. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 155,400,” amesema.
Leave a comment