Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya bahari na madini
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya bahari na madini

Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mavura
Spread the love

Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo kutoka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Togolani ameandika, “Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

Kwanza, Tanzania haijasaini mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu bahari wala madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Katika ziara hiyo, Rais Samia ameshuhudia utiwaji saini wa mkataba mmoja tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za Marekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.

“Mbali na mkataba huo, Rais Samia alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati.

“Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).  Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja,” amesema Mavura.

Pili, Mavura amesema Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandikwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul.

Amesema Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu.

“Mara ya kwanza dola za Marekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).

Ameongeza kuwa nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

“Tatu, tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo, si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka mitano.

“Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii,” ameandika Balozi Mavura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!