Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Baada ya Ruto, Museveni naye agoma kusaini muswada wa fedha
Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Baada ya Ruto, Museveni naye agoma kusaini muswada wa fedha

Rais Yoweri Museveni
Spread the love

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kutia saini Muswada wa Matumizi ya Pesa za Bajeti 2024 hadi Bunge la nchi hiyo litakaporejesha Sh750 bilioni zilizotengewa kwa ajili ya matumizi ya mipango muhimu ya serikali katika mwaka wa kifedha 2024/2025. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Rais Museveni alitakiwa kutia saini muswada huo jana Jumatano baada ya kukutana na Baraza la Mawaziri Ikulu ambapo alisisitiza vita yake dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za umma.

Msimamo huo mkali wa Rais Museveni unatishia utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa 2024/2025 na unaweka shughuli zilizopangwa hatarini kwa kuwa mwaka huu wa fedha utakamilika Juni 30, zikiwa zimesalia siku nne tu.

Muswada wa matumizi ya pesa za bajeti ni sheria yenye kiasi cha fedha kitakachotumiwa na kila wizara ya serikali, idara na serikali za mitaa, na kuidhinisha utoaji wa fedha hizo kutoka kwa Mfuko Mkuu wa Hazina.

Lengo la Muswada huo lilikuwa kutoa idhini ya matumizi ya umma kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Sh30.314 trilioni ili kukidhi matumizi ya mwaka unaoishia Juni 30, 2025, na kuidhinisha mahitaji yaliyotolewa na Bunge.

Spika wa bunge hilo, Anita Among, aliripotiwa kuwa hakupokea stakabadhi zinazoonyesha kutoridhishwa kwa Rais Museveni.

Hata hivyo, ikitokea kwamba Rais atarejesha Muswada huo kwa ajili ya kurekebishwa, Spika hatakuwa na suala lingine la kufanya ila kuurudisha bungeni baada ya wabunge kutoka mapumzikoni.

Bunge chini ya Ibara ya 79(1) ya Katiba ya nchi hiyo, lina uwezo wa kutunga sheria kuhusu suala lolote la amani, utulivu, maendeleo na utawala bora wa Uganda.

Katiba inampa rais siku 30 kuidhinisha Muswada huo. Hata hivyo, chini ya Kifungu cha 91(3) cha Katiba, Muswada unaweza kuwa sheria bila kibali cha rais iwapo ataurudisha Bbungeni mara mbili.

Wakati baadhi ya wabunge wakimtuhumu Rais Museveni kwa kujaribu kunyakua mamlaka ya kisheria ya Bunge katika mchakato wa kupanga bajeti, wengine walizungumzia tatizo la muda mrefu ambalo linahitaji kuzingatiwa haraka, wakitaja matumizi mabaya ya mamlaka ya ugawaji na ushawishi katika kamati ya Bajeti.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wilfred Niwagaba alieleza kuwa; “Bunge si taasisi ya mwisho na kwa kuzingatia Muswada huo, lina mamlaka ya kuuchunguza na kuufanyia marekebisho kama inavyofanya Miswada mingine,” alisema.

Aliongeza: “Kama Rais hataridhika, Ibara yote ya 91 ya Katiba ina maelezo ya kutosha kuhusu nini kitatokea, lakini hatimaye, Bunge lisipokubaliana na rais, basi litaiangalia upya muswada huo na hatimaye kuwa sheria chini ya Kifungu cha 91(6) na (7) cha sheria.”

Mapema mwezi huu, Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha Uganda, Ramathan Ggoobi, ambaye pia ni Katibu wa Hazina, aliwashutumu wabunge kwa kuvuruga Bajeti ya Kitaifa, kuhamisha na kuweka mahitaji yao katika maeneo bunge yao.

Hayo yanajiri baada ya muswada kama huo kuleta balaa nchini Kenya kwa vijana kuandamana na kuleta taharuki kubwa kiasi cha kumlazimu Rais wan chi hiyo, William Ruto kuurejesha bungeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!