Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko “Acheni kuwatumikisha watoto”
Habari Mchanganyiko

“Acheni kuwatumikisha watoto”

Spread the love

Wazazi na walezi Kijiji cha Ipapa Kata ya Ipunga Wilaya ya Mbozi mkoni Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwafanya watoto vitega uchumi vya kuendesha familia na kuwakoseha haki yao ya msingi ya kupata elimu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Wito huo umetolewa jana Jumanne na Polisi Kata ya Ipunga, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eletisia Mtweve alipokuwa anatoa elimu ya madhara ya ajira kwa watoto  aliowakuta kijijini hapo wakifanyishwa kazi za kiuchumi ili kuendesha familia zao.

“Ajira kwa watoto inaonesha unyonyaji kwa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima kuishi kwenye utoto wao, inawafanya washindwe kuhudhuria shule na inawaletea madhara ya kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili” alisema Mkaguzi Mtweve

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu katika jamii kwa kuyafikia makundi mbalimbali na kuwajengea uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu usalama ili jamii iache matendo maovu na kuuchukia uhalifu kwa usalama wa mali zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Tofauti kati ya Rais Ruto, Naibu wake zaanikwa

Spread the loveTOFAUTI za kimtizamo kati ya Rais William Ruto na Naibu...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CAG atoa kongole kwa PPAA

Spread the loveMDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...

error: Content is protected !!