Sunday , 7 July 2024
Home Kitengo Biashara TRC yafanya mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za treni za SGR
BiasharaHabari Mchanganyiko

TRC yafanya mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za treni za SGR

Treni SGR
Spread the love

Shirika la Reli Tanzania – TRC limetangaza mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za treni za reli ya kiwango cha kimataifa – SGR kati ya Dar es Salaam na Morogoro kuanzia tarehe 5 Julai 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taaria iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk imesema ongezeko la Safari litahusisha kuanza kwa treni mpya ya haraka (express train) ambayo itakuwa ikifanya safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro bila kusimama vituo vya kati.

Mabadiliko ya ratiba yatakuwa kama ifuatavyo; Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku. Treni itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 1:30 usiku.

Treni ya kawaida itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa 10:00 jjoni na itaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.

Abiria anashauriwa kukata tiketi kupitia njia ya mtandao https://sgrticket.tre.co.tz au madirisha ya tiketi yaliyo ndani ya vituo vya treni saa 2 kabla ya muda wa safari ili kuepuka msongamano.

Shirika litaendelea kuongeza idadi ya safari kulingana na ongezeko la idadi ya abiria ili kutoa huduma bora na za uhakika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mamilioni kwa kucheza kasino na sloti ya Sticky 777

Spread the love  Moja kati ya biashara nzuri na yenye mtaji mdogo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Spread the loveUamuzi wa Serikali ya Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa...

error: Content is protected !!