Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Chalamila achimba mkwara mzito Kariakoo, aapa kuwaonesha ‘show’
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Chalamila achimba mkwara mzito Kariakoo, aapa kuwaonesha ‘show’

Spread the love

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewathibitishia wafanyabiashara waliofungua maduka leo Jumatatu licha ya kuwepo kwa mgomo kwa baadhi yao, kwamba atakayejaribu kuwafanyia vurugu atamuonesha ‘show’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Yule atakayemletea mkwara aliyekubali kufungua, naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonyesha ‘show’ nzima. Kwa sababu mtu anakubali kufungua na wewe unamchimba mkwara, mimi ntakuchimba mkwara na hautainuka tena,” amesema.

Akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao leo Jumatatu, Chalamila amesema pamoja na uwepo kwa mgomo wa baadhi ya wafanyabishara, atalinda biashara zao na hawatafanyiwa vurugu.

RC Chalamila

Pamoja na mambo mengine, Chalamila amesema kero zilizopelekwa na wafanyabiashara hao serikalini zinaendelea kushughulikiwa.

Naye Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amelieleza Bunge kwamba tayari kamati ya wafanyabiashara hao inakutana na serikali hivyo, wabunge waliotaka kauli ya serikali kuhusu sakata hilo akiwamo Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) kuwa wawe na subira.

Wafanyabiashara hao wamegoma kuishinikiza Serikali kutatua changamoto zinazowakabili, ikiwemo kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mgomo huo umeibuka baada ya juzi Jumamosi kusambaa vipeperushi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa mgomo huo utakaoanza leo.

1 Comment

  • Hivi tukijiuliza tatizo ni nini hapo karihakoo? Utendaji, ufahamu, uelewa..! Kutoelewana au joto ya uchanguzi ujao?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lema: Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa

Spread the loveMJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kura mbili zamhamishia Mch. Msigwa CCM

Spread the loveAliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini na mjumbe wa zamani wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Spread the loveTanzania imeuza mahindi tani 650,000 nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji...

Habari za Siasa

Dk. Mpango, Ulega waongoza harambee ujenzi jengo la kitega uchumi CCM Pwani

Spread the loveMjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha...

error: Content is protected !!