Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Profesa Patrick Ndakidemi
Spread the love

Serikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi (CCM), wakulima kutumia njia mbadala ya matumizi ya madawa kwenye uzalishaji wa kahawa ikiwa pamoja na kupanda miche chotara ambayo inazalishwa na kusambazwa bure na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia imetoa wito kwa wazalishaji viuatilifu vya asili kujisili kwa sababu serikali imepanga kununua zaidi ya lita 20,000 katika mwaka ujao wa fedha.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alipokuwa anajibu swali la Prof. Ndakidemi.

Katika swali la msingi Prof. Ndakidemi alihoji ni lini Serikali itarejesha utoaji wa ruzuku ya pembejeo za dawa kwa Wakulima wa Kahawa. Kwenye maswali ya nyongeza alihoji lini serikali itafanyia ukarabati mifereji ikiwamo Makeresho uliopo Kata ya Kibosho Magharibi wilayani Moshi vijijini ili kuwezesha wakulima kpata maji ya uhakika kumwagilia kahawa.

Akijibu maswali hayo, Silinde amesema tayari mfereji huo ipo kwenye mipango ya bajeti ya wizara hiyo na sasa inamtafuta mkandarasi.

Aidha, amesema miche ambayo inazalishwa na kusambazwa kwa wakulima ina ukinzani na magojwa makuu ya kahawa ya chole buni na kutu ya majani ambayo ndiyo yaliyokuwa yanasababisha mahitaji ya matumizi makubwa ya madawa.

“Katika msimu wa 2023/2024, jumla ya miche 21,899,560 ilizalishwa na kusambazwa kwa wakulima wa kahawa katika mikoa yote inayozalisha kahawa nchini. Kati ya miche hiyo, mkoa wa Kilimanjaro ulipata miche 1,664,635 ambayo imesambazwa kwa wakulima ambapo, Wilaya ya Moshi imepata jumla ya miche 328,110 na kusambazwa kwa wakulima kupitia Vyama vya Ushirika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!