Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Guinea Bissau, Samia kuteta namna ya kudhibiti malaria
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Guinea Bissau, Samia kuteta namna ya kudhibiti malaria

Rais Umaro Sissoco Embaló
Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na Mwenyekiti wa Taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA), Umaro Sissoco Embaló anatarajiwa kufanya ziara nchini kwa lengo kujadili kwa kina namna ya kuendelea kupambana na kudhibiti ugonjwa hatari wa Malaria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwenyekiti huyo wa ALMA taasisi ambayo ilianzishwa mwaka 2009 na viongozi wa nchi zote 55 za Afrika kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030,  atafanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema pia ziara hiyo inalenga kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Guinea Bissau pamoja na kuibua maeneo ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kimkakati.

Ushirikiano huo utahusu uzalishaji wa zao la korosho, ushirikiano katika masuala yanayohusu udhibiti wa ugonjwa wa Malaria kupitia Taasisi ya ALMA, na ushirikiano katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Pia kupitia ziara hiyo Tanzania na Guinea Bissau zimedhamiria kuimarisha na kuinua kiwango cha ufanyaji biashara na uwekezaji hususan kupitia Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) ambapo nchi zote mbili zimeridhia uanzishwaji wa Eneo hilo.

“Itakumbukwa kuwa, wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwaka 2023, Mwenyekiti wa ALMA, Rais Umaro Sissoco Embaló alizitambua nchi saba ikiwemo Tanzania kwa kubuni matumizi bora ya Kadi ya Alama ya ALMA (ALMA Scorecard) inayosisitiza uwajibikaji na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

“Kupitia mpango huo, Tanzania ilitoa mafunzo kwa Wabunge, Viongozi mbalimbali na watoa huduma za Afya kuhusu namna ya kutumia kadi hiyo ya alama katika kuhamasisha uwajibikaji na utoaji elimu kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huo,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!