Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Mkuu Dk. Chidawali akemea mauaji ya albino
Habari Mchanganyiko

Askofu Mkuu Dk. Chidawali akemea mauaji ya albino

Askofu Dk. Daud Chidawali
Spread the love

 

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Gospel Christ Church Tanzania (GCCT) Dk. Daud Chidawali amekemea vikali vitendo vya baadhi ya watu wenye imani za kishilikini ambazo zinapelekea kukupoteza maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani maalubino. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Askofu huyo ametoa karipio hilo katika makao makuu ya kanisa hilo lililopo Meriwa Jijini Dodoma, kutokana na kuwepo kwa taarifa mbalimbazi za kutekwa kwa mtoto aliyefahamika kwa jina la Asimwe Mkoani Kagera aliyefanyiwa ukatili wa kupotezwa uhai wake pamoja na kukutwa ameondolewa viungo viungo.

Kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa hilo amesema kuwa vitendo vya kuwafanyia ukatili watu wenye ulemavu kwa kuwauwa na kuchukua viungo vyao ni masuala ya ushirikina na ni chukizo mbele za Mungu na ni aibu kwa taifa.

Akihubiri kakita ibada maalumu ya ufunguzi wa kongamano la maombi ya Usiku kucha kuchwa ya kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake amesema kuwa ni jambo la aibu kwa taifa la Tanzania ambalo linasifika kwa Amani na utulivu kujiusisha kwa Imani za kishirikina kwa kuwauwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Askofu Dk.Chidawali pia amewakemea watu wote kwa nafasi zao ambao wanatafuta vyeo,mali,uongozi au utajiri kwa kujihusisha na imani za ushirikina huku akiwataka kuwa ni lazima wawe na hofu ya Kimungu kwa ajili ya kufanya mambo yao kwa utukufu wa Mungu.

Akiendelea kukemea vitendo vya mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi amesema kama kuna wana siasa ambao wanajihusisha kwa vitendo hivyo wanatakiwa kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo nikumfanya Mungu achukie na kilipiga taifa kwa balaa.

Askofu Dk. Chidawali amesema kuwa uchumi wa nchi na maisha ya mwanadamu hauwezi kustawi kutokana na ushirikima bali uchumi unasimama kutokana na nguvu ya Kimungu.

Amesema hakuna maana yoyote kuwa na uchumi ambao unasababisha uzuni na uchungu kwa baadhi ya watu wenchine na kufanya hivyo ni machukizo mbele za Mungu.

Amesema kuwa iwapo watu watacha njia za Mungu na kumgeukia shetani kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji na kudanganywa kuwa wakiuwa watu watapata utajiri basi wajuwe wazi kuwa wanaenda kulifanya taifa kuwa kisiwa cha maombolezo na kilio cha kusaga meno.

Kutokana na kuwepo kwa matukio mbalimbali ya kutisha nchini Kanisa la GCC lililopo Meriwa Jijini Dodoma wameanzisha maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa pamoja na maadalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Pia kanisa linafanya maombi ya kitaifa kwa maana ya uchumi wa kitaifa, uchumi wa kanisa na uchumi wa mtu mmoja pamoja na kuwafanya wanaosimamia uchumi kuwa na hofu ya Mungu kwa manufaa ya wale wote wanao waongoza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!