Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti
Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaachia kwa masharti, Mkurugenzi wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, waliosota rumande kwa siku mbili, wakituhumiwa kusambaza taarifa za uchochezi mitandaoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakili wa watuhumiwa hao Hekima Mwasipu, akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, amesema Jacob na Malisa waliojisalimisha Polisi tarehe 25 Aprili mwaka huu, wameachwa kwa dhamana leo tarehe 27 Aprili 2024.

Wakili Mwasipu amedai, mbali ya kuachwa kwa dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja, Jacob na Malisa wametakiwa kuripoti Jumatatu ijayo majira ya saa 2 asubuhi.

“Wameachiwa kwa dhamana na wameambiwa waripoti Jumatatu asubuhi. Wamehojiwa kwa tuhuma za uchocheza na kusababisha taharuki kwenye jamii , pamoja na kosa la kusambaza taarifa za uongo kwa Jeshi la Polisi limeua raia,” amesema Wakili Mwasipu.

Tarehe 13 Aprili 2024, Jacob na Malisa kupitia katika akaunti zao za mitandao ya kijamii, walitoa taarifa zilizodai Robert Mushi (Babu G), ameuawa chini ya mikono ya Polisi na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam.

Kabla ya kuachiwa kwa dhamana, makundi mbalimbali yalipaza sauti kulitaka Jeshi la Polisi liwafikishe mahakamani au liwaache kwa dhamana, badala ya kuwaweka rumande kinyume cha sheria.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ulilaani tukio hilo likisema “tunasikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima dhamana ndugu Malisa na Jacob, kinyume na Sheria, huu ni ukiukwaji wa haki za watuhumiwa.”

“Hivyo, tunalisihi Jeshi la Polisi kuwaachia kwa dhamana. THRDC Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kuwaacha watanzania watumie uhuru wao kuhoji kupitia mitandao au kutoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii,” limesema tamko la THRDC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!