Monday , 20 May 2024
Home Kitengo Biashara EITI wakutana na kampuni za madini, gesi
Biashara

EITI wakutana na kampuni za madini, gesi

Spread the love

Ujumbe kutoka Asasi ya Umoja wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) ukiongozwa Katibu Mtendaji, Mark Robinson na umekutana na wawakilishi wa Kampuni za Madini na Gesi na mashirika ya Umma ya TPDC na Stamico kujadili utekelezaji wa shughuli za EITI nchini.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maeneo yaliyolengwa katika majadiliano hayo yaliyofanyika jana Alhamisi jijini Dar es Salaam, ni ushiriki wa kampuni na mashirika ya Umma (SOEs) yanayofanya shughuli za uziduaji katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya mwaka 2023 ( EITI Standard 2023).

Mapitio ya matokeo ya tathmini ya mwaka 2023 ambapo masuala yafuatayo yalipendekezwa kuboreshwa ili Tanzania ifanye vizuri katika tathmini ijayo ya mwaka 2027, uwekaji wazi wa mikataba ya madini na gesi asilia na uwekaji wazi wa wamiliki wanufaika katika kampuni za madini, mafuta na gesi asilia.

Mchango wa wachimbaji wadogo na urasimishaji wa sekta ya uchimbaji mdogo.

Ushiriki wa kampuni na SOEs katika utekelezaji wa vigezo vipya vilivyoongezwa (EITI Standard 2023). Vigezo hivyo ni pamoja na masuala ya kuzuia rusha, jinsia na mazingira na Energy Transition.

Aidha, katika majadiliano hayo, ilielezwa kuwa baadhi ya kampuni tayari zimeweka wazi mikataba yake kupitia masoko ya hisa na hivyo iko wazi kwa umma.

Pia ilielezwa kuwa uwekaji wazi mikataba utasaidia kuhamasisha uwazi na wananchi kujua faida kutoka katika uvunaji wa rasilimali madini mafuta na  gesi.

Wawakilishi watatoa ushirikiano kwa Sekretariati ya EITI Tanzania katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya mwaka 2023.

Pia, Wawakilishi wa kampuni na mashirika waliohudhuria ni pamoja na Pan Africa Energy, Maurel & Prom, Tanzania Chamber of Mines, Tembo Nickel, Shanta Gold Mine, TPDC na Stamico.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

error: Content is protected !!