Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtoto atolewa skrubu iliyokwama kwenye mapafu
Habari Mchanganyiko

Mtoto atolewa skrubu iliyokwama kwenye mapafu

Spread the love

Mtoto mwingine ametolewa Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera kilichokwenda kuinasa na kisha kuitoa.

Mtoto huyo anadaiwa alikua akiichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Mwanaada Kilima amesema mtoto huyo alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa sana na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.

Mzazi wa mtoto huyo, Msafiri Chatanda amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tangu alipofikishwa hospitali hapo na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.

Chatanda amewaasa wazazi kuwa watoto wamekuwa na desturi ya kuchezea vitu lakini hakuna mzazi anahangaika kumkumbusha mtoto madhara yake na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.

Katikati ya mwezi huu, Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lilifanikiwa kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Aidha, mapema jana Jumatatu, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dk. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!