Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang
Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole kwa wananchi wa Hanang waliofikwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha vifo na majeruhi huku ikitumia nafasi hiyo kukabidhi mitungi ya gesi 200 yenye ujazo wa kilo 15 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo kupata nishati safi ya kupikia. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mitungi hiyo ya gesi na majiko yake ambayo imetolewa naql Oryx imekabidhiwa kwa Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu,Jenista Mhagama ( kushoto) akiwa akimshukuru Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Oryx Gas Tanzania, Shaban Fundi (kulia) baada ya Oryx kukabidhi mitungi 200 ya kilo 15 yakiwa na majiko yake kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh.

Akizungumza wakati wa kupokea mitungi hiyo Mhagama ameishukuru kampuni ya Oryx kwa mchango wake kwa wananchi wa Hanang kwani umekuja wakati muafaka kusaidia wananchi hao kwa kuwapatia nishati safi ya kupikia katika wakati huu mgumu.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mauzo Oryx Gas, Shaban Fundi amesema kampuni hiyo imefika Hanang eneo la Katesh kuungana na kuwapa pole watanzania wenzao waliofikwa na janga la mafuriko na maporomoko.

“Tunajua kwa hakika wenzetu wameathirika sana katika kipindi hiki ni gharama kubwa kupata vyanzo vya moto kupikia. Oryx Gas tumekuja kukabidhi majiko 200 na mitungi ya gas ujazo wa kilo 15 kwa waathirika wa tukio hili.

“Oryx Gas tunawaombea marehemu wapumzike kwa amani, zaidi tunawaombea majeruhi wote wapone haraka na werejee katika majukumu yao ya kila siku.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

error: Content is protected !!