Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang
Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the love

KAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil na Camel Cement zimekabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbali na kukabidhi hundi hiyo pia Kampuni ya Camel Oil imetoa misaada mbalimbali kama Magodoro, maji na mablanketi kwa ajili ya waathirika hao na hiyo ni sehemu ya kampuni kurejesha tabasamu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya milioni 100 pamoja na mahitaji hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha na msaada huo vifaa hivyo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

“Tumepokea Sh.milioni 100 kutoka Camel Cement lakini na vitu vingine kutoka Camel Oil na tunaomba kwa niaba ya Serikali mtupelekee salamu kwa menejiment tunashukuru.

“Bado tunahitaji misaada ya kibinadamu ili kuwezesha ufumbuzi wa muda na wa kudumu kwa ajili ya ndugu zetu ili maisha yarejee kama kawaida ” amesema Waziri Jenista.

Awali wakati abakabidhi misaada hiyo Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma wa Amsons Group, Bhoke Rioba amesema Camel Cement imeweka fedha kwenye akaunti ya maafa ya Serikali kiasi cha Sh.milioni 100,  magodoro 100 pamoja na mashuka 100.

Amesema kutoa kwao fedha na msaada huo ni muendelezo wa kampuni hizo kwenye kampeni yake ya kurudisha tabasamu kwa jamii ya Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!