Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kasekenya akagua miundombinu Songwe kukabili El-nino
Habari Mchanganyiko

Kasekenya akagua miundombinu Songwe kukabili El-nino

Spread the love

 

WAKALA wa Bararabara Tanzania (TANROADS) mkoani Songwe umewahakikishia wananchi kuwa umejipanga kukabiliana na mvua za El-nino kwa kukamilisha kwa wakati ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja ili kukwepa madhara yasiyokuwa na tija. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TANROADS mkoani Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga mbele ya Naibu Waziri wa ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya aliyefanya ziara ya kukagua barabara zilizotengenezwa na TANROADS.

Ukaguzi huo uliofanywa jana ulilenga kutathmini na namna mkoa ullivyojiandaa kuepuka madhara yatokanayo na mvua hizo zinazotarajiwa kunyesha katika msimu huu wa vuli.

Katika ukaguzi wake Mhandisi Kasekenya alianza wilaya ya Songwe ambako alikagua daraja la Galula katika mto Songwe, barabara inayoanzia kijiji cha Galula hadi Muheza na kuunganisha wilaya ya Songwe na makao makuu ya mkoa.

Pia alikagua eneo hatarishi kwa mafuriko lililopo bonde la mto Zila lenye urefu wa kilometa tano katika barabara inayoanzia Mbalizi kupitia Mkwajuni-Saza hadi Makongorosi na kutoa maagizo kwa wakandarasi kujenga kwa kuzingatia ufanisi.

Aidha, Mhandisi Bishanga amesema daraja la Galula lililoanza kujengwa tangu mwaka 2015/16, litaendelea kujengwa wiki ijayo baada ya kufanyika usanifu upya wa kulaza vyuma na kuweka zege juu.

Akiwa kwenye bonde la mto Zila amesema serikali imeleta fedha za kuinua tuta kwenye barabara hiyo na kuongeza upana na kuwa amejipanga kujenga kwa ufanisi kuzuia kasi ya maji, kazi itakayoanza wiki ijayo.

Amesema eneo hilo la Mto Zila limekuwa likileta maafa kwa wananchi na mifugo takribani miaka mitatu mfululizo hali iliyoumiza vichwa viongozi wa serikali na hatimaye Serikali kutoa fedha kuhakikisha eneo linadhibitiwa kuhepuka maafa.

Pamoja na maelezo hayo, Naibu Waziri amesisitiza kuhakikisha barabara zote zinasafishwa kabla ya mvua hazijaanza kunyesha ili kuepuka kero ya kutuama kwa maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!