Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Manara amvaa Makonda
Habari Mchanganyiko

Manara amvaa Makonda

Paul Makonda
Spread the love

 

SAKATA la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudai kuna makundi yanataka kumuua ama kumfikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka, Msemaji wa Klabu wa Yanga, Haji Manara amemuikukia na kumshushia tuhuma nzito. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makonda ameibua madai hayo jana Jumatatu, tarehe 11 Aprili 2022 kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram akisema mkakati huo unaratibiwa na makundi matano yenye lengo la kuangamizi maisha yake.

Aliyataja makundi hayo ni wauza dawa za kulevya, wanufaika na dawa za kulevya, wapenzi wa jinsia moja ‘mashoga,’ wanaokesha usiku kucha kutafuta kulipa kisasi kwa wasaidizi wa Dk. Magufuli na waliowahi kuwa sehemu….

“Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi,” aliandika Makonda

Katika andishi hilo, Makonda alisema “mambo mawili najiuliza. Pamoja na kazi zote nzuri nilizozifanya kwa chama changu (CCM), serikali yangu na wananchi wa Dar haya ndiyo malipo yake?

“Mtu aliejenga hospitali, aliejenga ofisi za CCM, magari ya polisi, ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha Serikali na viongozi wa Dini. Leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa,” alisema

Akihitimisha andiko lake, Makonda alisema “pamoja na kwamba lipo kundi kwenye mitandao linalolipwa ili kuwaanda Watanzania pale watakapo nikamata ionekane ni sawa.”

“Hakika ipo siku walemavu, yatima, wajane na waliotamani watoto wao wasife kwa dawa za kulevya sauti zao zitasikika. #Ukiona maji yametulia jua kina nikirefu.”

Haji Manara

Hadi leo Jumanne tarehe 12 Aprili 2022, saa 4:30 asubuhi ujumbe huo wa Makonda alioweka na kipande cha sauti kimesikilizwa na watu zaidi ya 208,620 pamoja na kuchangiwa na zaidi ya watu 7,101 akiwemo Manara.

Akichangia ujumbe huo, Manara ameandika, “anaitwa Mungu, mkweli na kwa sasa hachelewi kujibu, leo unatafuta sympathy huku ukijua nn ulwafanyia watu? Dhulma, dharau, kejeli, matusi na hata kuwaona viongozi wenzio hawana maana.”

“Ukawabambizia kesi za unga watu, ukanyang’anya watu magari yao, sisahau siku uliyokataa kukaa jukwaani pale kwa Mkapa na kukaa ktk benchi kama kocha kisa hutaki kusalimiana na mkubwa wako eti kisa hakupendi.”

Manara ameendelea kusema, “umesahau hata mtoto wa mkubwa ukasema anauza unga na kutaka kumchafua kisa ulipata cheo? Acha kumsingizia Mungu, waombe msamaha Watanzania kwa dhulma zako na usitegemee Serikali ikuonee huruma.”

“Inajua everything about you, kina sudi ukawasweka ndani bila sababu, mm ndio nilikuwa mnyonge wako, hebu kwenda zako, akuue nani ww? Utajiua kwa stress zako mwenyew, cheo huna nenda kolomije kavue sangara.”

Mwandishi na mchambuzi mwandamizi wa michezo, Edo Kumwembe yeye ameweka emoji cha kucheka, “😂😂😂😂😂😂😂.” Huku
van_tanzania akisema “wapumbavu wote hao na mwisho wa siku watakufa wao we utabaki.”

joelmakinga amesema, “Mungu ni mwaminifu hakuna jaribu lisilokuwa na mlango wa kutokea naamini sauti yako itasikika na Mungu atatenda kwa wakati. Wewe kwangu ni mmoja wa viongozi ninaowapenda hauna makandokando usichoke kupamabana.”

princesangola8789 amechangia akisema “kuna vitu naungana naww mengine apa ulikuwa unafanya vitu vya honyoo sana lamda tu ungesema kuwa nilipo kosea nisameheni ningekuelewa.”

rehemakandimwa2 yeye amesema “we ulitangaza akuna mtu anaekula raha hapa duniani wewe no moja sasa unalia nn kaka hii ndio tanzania, pole.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

error: Content is protected !!