Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Mkude ang’atuka Jimbo la Morogoro
Habari Mchanganyiko

Askofu Mkude ang’atuka Jimbo la Morogoro

Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro nchini Tanzania, Telesphor Mkude
Spread the love

BABA Mtakatifu Francisko, ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro nchini Tanzania, Telesphor Mkude la kung’atuka madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Papa Francisko ameridhia ombi hilo la Askofu Mkude, jana Jumatano tarehe 30 Desemba 2020, baada ya kuwaongoza, kuwatakatifuza na kuwafundisha watu wa Mungu kama Padre kwa miaka 48 hadi kufikia mwaka 2020 na miaka 32 kama Askofu Jimbo.

Tangu tarehe 12 Februari 2019, majukumu yote ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu jimbo hilo la Morogoro yamekuwa yakisimamiwa na Monsinyo Lazarus Vitalis Msimbe aliyeteulia na Papa Francisko ili kutoa nafasi kwa Askofu Mkude kushughulikia zaidi afya yake.

Askofu Mkude alizaliwa tarehe 30 Novemba 1945 eneo la Pinde, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Baada ya safari yake ya kimasomo, tarehe 16 Julai 1972, Mkude alipewa daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Morogoro.

Tarehe 18 Januari 1988, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga na kuwekwa wakfu tarehe 26 Aprili 1988 na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Ilipogota tarehe 5 Aprili 1993, tena Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro hadi Jumatano ya tarehe 30 Desemba 2020, Baba Mtakatifu Francisko aliporidhia ombi la kung’atuka kwake kutoka madarakani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!