Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbaroni kwa kumchoma mtoto moto
Habari Mchanganyiko

Mbaroni kwa kumchoma mtoto moto

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei
Spread the love

WATU wawili, Judith Amoni Mwansansu (39) Mkazi wa Mwanjelwa na Aive Alex Swalo (17) Mkazi wa Mwanjelwa Mtaa wa Soko wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto wa miaka sita. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 1 Agosti, 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema tukio hilo lilifanyika jana majira ya saa tatu usiku ambapo jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema, ya kwamba mtoto huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali kwa moto.

“Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mhanga alikuwa ameenda kucheza na rafiki zake na aliporudi nyumbani majira ya jioni ndipo shangazi yake alimuadhibu kwa kumchapa na waya wa umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha na maumivu makali mwilini,” amesema Kamanda Matei na kuongeza.

“ Inadaiwa kuwa tarehe 01.08.2018 majira ya asubuhi, watuhumiwa waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto huyo kwa kumuunguza kwa moto sehemu za miguuni na kwenye makalio.”

Kamanda Matei amesema Mhanga amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi ya kitabibu huku watuhumiwa wote wawili wamekamatwa kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!