Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vifaa vya upekuzi, kamera za CCTV kufungwa magerezani
Habari Mchanganyiko

Vifaa vya upekuzi, kamera za CCTV kufungwa magerezani

CCTV Camera
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema, inakusudia kuongeza vifaa vya upekuzi magerezani na kufunga kamera za CCTV ili kubaini matendo maovu yanayofanyika ndani ya magerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 26 Mei, 2020 na waziri wa mambo ya ndani wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Rukia Kassim Ahamed.

Rukia  ameuliza Je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia vitendo viovu na vibaya Magerezani.

Majibu ya waziri wa mambo ya ndani aliyoyatuma kwa njia ya mtandao yanasema, Jeshi la Magereza ni chombo pekee cha Serikali chenye dhamana kisheria kuwapokea na kuwahifadhi wahalifu wa aina zote wanaoletwa magerezani kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Amesema, pamoja na ukweli kwamba nyakati kadhaa kumekuwepo na vitendo viovu magerezani mathalani; askari kuwa na mahusiano mabaya na mfungwa, uingizaji wa vitu visivyoruhusiwa magerezani, matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya wafungwa, wafungwa kujaribu kutoroka, kupigana, kutoeleana lugha za matusi, kuharibu mali ya gereza na vitendo hivyo vimekuwa vikidhibitiwa kwa mujibu wa Sheria.

Waziri huyo amesema, kanuni na taratibu zilizopo za magereza nazo ni:-

(i)   Sheria ya Magereza ya Mwaka 1967 (The Prison Act of 1967)

(ii)  Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997 (The Prisons Service Regulations of 1997)

(iii) Kanuni za makosa Magerezani (The Prison (Prison Offences Regulations)

(iv)Kanuni za kudumu za Jeshi la Magereza, Toleo la 4 la Mwaka 2003 (Prisons Standing Order)

Aidha, sheria na kanuni tajwa zimeainisha aina ya makosa, hatua na adhabu zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya afisa/askari wa Magereza na mfungwa/mahabusu pale inapothibitika amefanya vitendo hivyo gerezani.

 “Hivyo, mpango ambao Serikali kupitia Jeshi la Magereza imekuwa nao ni kuongeza vifaa vya upekuzi Magerezani (Ditectors) na kufunga CCTV – Kamera Magerezani ili kubaini matendo maovu.”

“Pia, kuendelea kufuata sheria na kanuni tajwa ambazo zilipitishwa na Bunge lako Tukufu na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaohusika na kufanya vitendo viovu magerezani,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!