Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba, Yanga zapigwa faini kwa kutumia mlango usio rasmi
Michezo

Simba, Yanga zapigwa faini kwa kutumia mlango usio rasmi

Spread the love

KAMATI ya uendeshaji Ligi Kuu Tanzania Bara (kamati ya saa 72) imezitoza faini klabu za Simba na Yanga kwa makosa ya kutumia milango isiyo rasmi kwenye mchezo uliowakutanisha miamba hiyo Februari 16, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Simba imepigwa faini ya shilingi 3 milioni kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mchezo huo, huku Yanga ikitozwa faini ya shilingi 6 milioni sambamba na kosa la kutoingia vyumbani siku ya mchezo huo.

Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ameeleza kuwa kamati itatoa adhabu kali kwa timu ambayo haitatumia milango iliyo rasmi kuingia uwanjani kwa sabu ya kulinda hadhi ya Ligi hiyo.

“Ukifanya utafiti leo asilimia 65 ya mapato kwenye mpira wa miguu yanapatikana kwenye haki za matangazo ya televisheni na watu tulio wauzia haki hiyo wanakaa kwenye njia rasmi ili wasubiri timu ziingie halafu wanakwenda kupitia kwengine” alisema Wambura

Timu zote mbili hazikutumia mlango uliozoeleka na badala yake kutumia milango iliyopembeni na uwanja huo kutokana na kuhusisha na imani za kishirikina na mchezo huo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika hatua nyingine klabu ya Yanga ilipigwa tena faini ya shilingi 1 milioni baada ya kufanya tena kosa kama hilo la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya Jkt Tanzania.

Tazama video kamili hapo chini

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!