Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Mafaili’ wagombea ubunge mikononi mwa Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

‘Mafaili’ wagombea ubunge mikononi mwa Magufuli

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli ameongoza kikao cha kamati kuu ya chama hicho Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Kikao hicho kimefanyika leo Jumanne tarehe 18 Agosti, 2020 kikiwa na ajenga ya kupendekeza kwa kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho majina ya wagombea ubunge wa majimbo na wabunge wa viti maalum.

Picha za mnato zinaonyesha wajumbe wa kikao hicho wakisoma nyaraka mbalimbali ambazo ni mapendekezo ya vikao vya awali vya mchunjo ngazi ya wilaya, mikoa na sekretarieti ya kamati kuu.

Katika picha hizo, mzigo wa ‘mafaili’ yanaonekana mezani kwa Rais Magufuli.

Kamati Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally amewataka wale wote walioshiriki kura za maoni kurejea katika majimbo yao ili pindi majina yatakapoteuliwa, waanze mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu.

Tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekwisha kuanza kutoa fomu za kugombea ubunge tangu tarehe 5 Agosti na litahitimishwa 25 Agosti, 2020.

Wagombea wa vyama mbalimbali wamekwisha kuanza kuchukua fomu hizo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole mara kadhaa amenukuliwa na vyombo vya habari akisema, chama hicho ‘kitawakata’ wale wote waliojihusisha na rushwa wakati wa kura za maoni.

Polepole alisema, “kama wewe unajua hukujihusisha na vitendo vya rushwa, kaa na kuwa na amani kabisa, lakini kama ulihusika tutakufanyia ‘surprise’ ambayo hukuitegemea.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!