Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Gambo: Kenya inataka kuua utalii wa Tanzania
Habari za Siasa

Gambo: Kenya inataka kuua utalii wa Tanzania

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini (CCM)
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Arusha (RC), Mrisho Gambo amesema, Serikali ya Kenya inakata kutumia ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) kuua utalii wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Gambo amesema hayo leo Jumatano tarehe 20 Mei, 2020 kupitia taarifa yake kwa umma inayoelezea hali ya maambukizi ya corona kwenye mkapa wa Tanzania na Kenya uliopo Namanga.

Taarifa hiyo ya Gambo, ameitoa ikiwa ni siku nne zimepita, tangu Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alipotangaza kufunga mpaka wa huo wa Namanga pamoja na unaounganisha Kenya na Somalia kwa siku 30 kuanzia tarehe 16 Mei, 2020.

Rais Kenyatta alisema kulikuwa na ongezeko la wagonjwa wa corona kutoka nje ya Kenya ikiwamo watu wanaoingia akitolea mfano wagonjwa 43 waliovuka mipaka ya Tanzania na Somalia walibainika kuwa na corona.

Katika taarifa aliyoitoa Gambo, imeelezea jinsi mkakati wa mkoa huo unavyoshughulikia kujikinga na maambukizo ya corona akisema mkoa wake umeona umuhimu wa kuanzisha utaratibu wa kuchukua sampuli na kuwapima madereva wa malori yanayopita mpaka wa Namanga wakitokea Kenya.

Amesema, sampuli zote zinazochukuliwa na wataalam wa afya, zimekuwa zinapelekwa Maabara Kuu ya Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya kupata majibu ya vipimo husika.

“Tumechukua uamuzi huu ili kuwalinda wananchi wetu na maambukizi ya COVID-19 kutoka nchi hiyo (Kenya) ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa afya ya wananchi wetu kama sehemu ya maandalizi ya kupokea watalii msimu utakapoanza mwezi Juni 2020,” amesema Gambo.

Amesema, utaratibu wa kuchukua sampuli za COVID-19 kwa madereva wanaotoka Kenya ulianza kutumika tarehe 14 Mei, 2020 na sampluli zilichukuliwa tarehe 14,16 na 18 Mei, 2020.

 Akizungumzia matokeo ya vipimo, Gambo amesema, madereva 44 toka Kenya walichukuliwa vipimo tarehe 14 Mei, 2020 na majibu yalitoka tarehe 16 Mei, 2020 na matokeo ya vipimo ni kuwa madereva 14 (11 Wakenya, 1 Mganda na 2 kutoka nchi ambayo tunaihifadhi)kutoka upande wa Kenya walikuwa “Positive” (wana corona)na 30 walikuwa “Negative” (hawana corona).

Amesema, tarehe 16 Mei, 2020 madereva 23 toka Kenya walichukuliwa vipimo na tarehe 19 Mei, 2020 majibu yalikuwa 10 ni “Positive.’ (wote kutoka nchi ya Kenya) na 13 ni “Negative.”

Gambo amesema, tarehee 18 Mei, 2020, madereva 11 kutoka Kenya walichukuliwa vipimo na majibu yatatangazwa mara baada ya kupatikana kutoka Maabara Kuu ya Taifa Dar es Salaam.

“Aidha, ili kujiridhisha tulichukua upya sampuli ya baadhi ya madereva (sampuli zilichukullwa kwa madereva 19) waliotoka Tanzania na kupimwa mpakani Namanga upande wa Kenya na kutangazwa na nchi ya Kenya kuwa ni “Positive” amesema Gambo

“Sampuli hizi baada ya kupelekwa maabara Kuu ya Taifa Dar es Salaam zilionyesha kuwa madereva hao waliotoka Tanzania ni “Negative.”

Gambo amesema, “Mkoa wa Arusha umejiridhisha kuwa hizi ni mbinu za nchi ya Kenya ili kuua soko la utalii mkoani Arusha na Tanzania kwa ujumla.”

“Madereva wanaoonekana kuwa ni “Positive’ hawaruhusiwi kuvuka mpaka kuingia Tanzania wala kwenda Kenya. Mkoa wa Arusha unaendelea kuchukua tahadhari na kudhibiti maambuklzi ya Covid-19 kupitia mpaka wa Namanga jirani na Kenya,” amesema.

Amesema, wanaendelea kushukuru kwa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa majirani zao Wakenya katika mpaka huo wa Namanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!