Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ahadi nzito ya ACT-Wazalendo 2020 – 2025
Habari za Siasa

Ahadi nzito ya ACT-Wazalendo 2020 – 2025

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo endapo kitachaguliwa kuongoza Serikali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, kimeahidi kuunda ‘Timu ya Majaji’ ili kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo watu kupotea, kutekwa na kuuawa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 na Idrisa Koweta, Katibu wa Sera wa chama hicho wakati akisoma muhtasari wa Ilani ya Uchaguzi ya ACT-Wazalendo katika uzinduzi wa ilani hiyo, jijini Dar es Salaam.

“Uhuru, Haki na Demokrasia, hili ni eneo la kwanza ambapo ilani hii inaonesha kwamba itafuta sheria zote kandamizi, itaunda Timu ya Majaji kuchunguza matukio yote ya utekaji, mauaji na watu kupotea, kulipishwa fidia na kufutia jinai,” amesema Koweta.

Muhtasari wa ilani hiyo umeonesha, kwamba kama ACT-Wazalendo kitashinda Uchaguzi Mkuu, serikali yake itasimamia Uhuru, Haki na Demokrasia kwa kufuta sheria kandamizi.
Ilani hiyo imeeleza, kwamba serikali yake itaimarisha taasisi za usimamizi wa uwajibikaji ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Na kwamba, kwenye Ilani hiyo Serikali ya ACT-Wazalendo itafufua mchakato wa Katiba Mpya pamoja na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Chama cha ACT-Wazalendo kimezindua Ilani yake ya uchaguzi baada ya wagombea wake katika kiti cha Urais wa Tanzania na Makamu wa Urais kupitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea nafasi hizo.

Wagombea wa chama hicho ngazi ya urais Tanzania Bara ni Benard Membe, mgombea mwenza wake ni Prof. Omary Fakhi, mgombea wake mwenza. Visiwani Zanzibar, mgombea urais wa chama hicho ni Maalim Seuf Sharif Hamad.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!