Thursday , 4 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Chana aagiza RITA kutoa elimu ya wosia, mirathi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waziri Chana aagiza RITA kutoa elimu ya wosia, mirathi

Dk.Pindi Chana
Spread the love

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Balozi Dk.Pindi Chana ameagiza ofisi za wakala wa usajili ufilisi na udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi za Makatibu Tawala wilaya zote za Tanzania bara kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuandika wosia kabla ya mauti ili kupunguza migogoro ambayo hutokeza mara baada ya wazazi kufariki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe… (endelea).

Dk. Chana ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa makatibu tawala kutoka mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Songwe ambapo alisema dhamira ya serikali ni kuona wananchi wanaishi kwa amani bila migogoro.

“Mafunzo ya leo yamejumuisha huduma za Vizazi na Udhamini lakini natoa wito ikiwezekana pia wafundishwe masuala ya Mirathi na Wosia kwani itasaidia kutatua migogolo sambamba na kuwasaidia wananchi namna ya kupata haki zao,” alisisitiza Waziri Chana.

Alisema kumekuwa na changamoto nyingi za masuala ya wajane na warithi halali kudhulumiwa mali zao baada ya mzazi mmoja hasa baba kufariki hivyo kupitia mafunzo hayo yaliyotolewa na rita yataenda kuleta matokea chanya katika kutatua migogoro.

“Msingi mkuu wa matatizo ya mirathi ni wazazi kutoandika wosia hivyo tutumie fursa tunazozipata za kukutana na wananchi kuwashauri waandike wosia ili kulinda haki za warithi halali na pia  tuwasisitize wananchi wafanye kazi sio kusubiri ndugu afe ili arithi mali hata kama yeye sio mmoja ya warithi wanaotambulika kisheria,” alisema Waziri Chana.

Kwa upande wake Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi alisema RITA imekuwa ikiandaa  mafunzo na mikutano kwa makundi mbalimbali  ya wadau wa maendelo na taasisi za serikali lengo ikiwa ni kuwapa uelewa wa huduma wanazozitoa sambamba  na  kujadiliana njia mbalimbali zitakazowezesha kuongeza ufanisi.

“Sheria ya Usajili wa vizazi na vifo inamtambua Katibu Tawala wa Wilaya kama msajili wa wilaya na huduma zinapatikana katika Ofisi zao hivyo wanahusika moja kwa moja  na usajili wa vizazi,vifo na ndoa lakini pia wanafuatilia na kukusanya taarifa za hukumu za masuala ya Talaka katika maeneo yao,” alisema Kanyusi.

Aidha, Kanyusi  alisema Ofisi za Makatibu  Tawala wa Wilaya ni mahali ambapo wafungishaji ndoa wanapata shahada za kufungisha ndoa na ikumbukwe hivi karibuni RITA imewataka wafungishaji ndoa wote  kujisajili  katika mfumo wa eRITA kwa ajili ya kupata Leseni mpya za kidijitali.

Katika kikao hiki tutajadili na kuweka mikakati ya kulisimamia agizo hili kwani ni la msingi katika uratibu wa huduma ya usajili wa ndoa.

Kanyusi  aluongeza kuwa matumizi ya teknolojia yameendelea kushika kasi katika kuboresha mifumo ya kuwahudumia wananchi, kupitia  mfumo huu mwananchi anaweza kutuma maombi ya usajili kielektroniki bila kufika ofisi za wakala.

Naye miongozi mwa washiriki wa mafunzo hayo, Katibu Tawala Wilaya ya Makete, Grace Mgeni alisema kupitia mfumo wa eRITA utasaidia kufikia idadi kubwa ya wananchi na hivyo kupunguza msongamano kwenye ofisi sambamba na kuokoa muda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka Watanzania kulinda viumbe hai baharini

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Waingereza kuifuta historia ya Conservatives leo?

Spread the loveWaingereza milioni 50 wanatarajiwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu leo...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Biden agoma kujitoa uchaguzi Novemba, aangukia pua kura za maoni

Spread the loveRAIS wa Marekani, Joe Biden amekataa kujitoa kwenye uchaguzi wa...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia, Nyusi wapongeza mkakati wa utanuzi PBZ, yakaribishwa kufungua tawi Msumbiji

Spread the loveRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na...

error: Content is protected !!