Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana kupitia njia ya mtandao tarehe 7 Juni mwaka huu katika Mkutano wa 23 wa Jumuiya hiyo yenye nchi wanachama nane. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Moja ya ajenda ya mkutano huo ni kupitishwa kwa Veronica Mueni Nduva kuwa Katibu Mkuu mpya wa EAC.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano wa Mawasiliano ya Umma kutoka Jumuiya hiyo, Simon Owaka, kikao hicho, ambacho kitakuwa chini ya uenyekiti wa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini, pia kitapitisha jina la Jaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), ambaye pia anatoka Kenya.
![](https://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2024/06/Screenshot-2024-06-05-at-03.49.30.png)
Serikali ya Kenya imependekeza jina la Veronica Mueni Nduva kuchukua nafasi ya Caroline Mwende Mueke katika nafasi ya Katibu Mkuu wa EAC.
Ikumbukwe kuwa, jina la Mueke lilipendekezwa na Rais wa Kenya, William Ruto kama mbadala wa Peter Mutuku Mathuki, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Urusi.
Mueke alitarajiwa kumaliza kipinchi cha miaka miwili cha uongozi wa mtangulizi wake.
Hata hivyo, tarehe 15 Aprili 2024, Serikali ya Kenya ilipitisha jina la Veronica Mueni Mwende kama mbadala wa Mweke ndani ya EAC.
Kwa mujibu wa kifungu hicho cha sheria, Katibu Mkuu wa EAC, anapaswa kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Hata hivyo, Mathuki alikuwa amehudumu kwa miaka mitatu, katika nafasi hiyo ya juu ndani ya EAC, kabla ya maamuzi ya tarehe 8 Machi 2024, yaliyofikiwa na Rais Ruto.
Kulingana na itifaki ya kuanzisha EAC, Rais wa nchi husika anaweza kupendekeza jina kwa nafasi ya Katibu Mkuu, kabla ya kuidhinishwa na Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.
Leave a comment