Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge wanawake, Oryx wampa tuzo Rais Samia kuhamasisha nishati safi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wabunge wanawake, Oryx wampa tuzo Rais Samia kuhamasisha nishati safi

Spread the love

WABUNGE wanawake kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania wametoa tuzo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Tuzo hiyo kwa Rais Samia imetolewa leo Ijumaa Mjini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi Kupikia Duniani ambapo Oryx imeshirikiana na wabunge hao pamoja na wabunge wanaume ambao ni vinara katika nishati safi.

Katika maadhimisho hayo Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ametoa sababu za Rais Samia kupewa tuzo ya kumtambua Rais kama kinara wa nishati safi nchini, Afrika na duniani kwa ujuma.

Dk. Tulia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema wanampongeza rais kwa kuwa kinara wa nshati safi ya kupikia.

Amesema Rais Samia alipokuwa Dubai na hivi karibuni alipoenda katika mkutano uliofanyika Paris ametambulika na dunia nzima kama kinara wa nishati safi ya kupikia. Hivyo wanaendelea kusisitiza Rais Samia ndiye kinara wa nishati safi ya kupikia.


Amesema katika Bara la letu la Afrika kuna changamoto ya nishati ya kupikia na takwimu zinaonesha asilimia 90 barani Afrika wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na ili kutoka katika nishati hiyo na kurudi katika sifrui kabisa itachukua muda.

Hivyo, Rais Dk.Samia anasaidia kuupunguza muda kwa kuendelea kutafuta fursa kubadilisha upikaji kwa kuacha kutumia nishati chafu na kuhamia katika nishati safi ya kupikia kama gesi.

Aidha, amesema juhudi hizo za rais zimeanza hapa nchini Tanzania na takwimu nchini zinaonesha asilimia 90 za wananchi mpaka sasa wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na juhudi za Rais zinatusogeza angalau kutoka asilimia 90 na kusogea mpaka 25 ili wawe wachache wanaotumia nishati chafu ya kupikia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema katika kutambua mchango wa Rais Samia katika nishati safi wameamua kutoa tuzo kwa Rais kama sehemu ya kumuunga mkono kwa juhudi anazofanya.

Amesisitiza mpaka sasa wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake 35000 kwa makundi mbalimbali nchini na wataendelea na mkakati wao kwani dhamira yao ni kuona asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2032 kama ambavyo Rais Samia ameelekeza.

Awali Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake nchini, Shally Raymond amesema wabunge wanawake pamoja na wabunge vinara wa nishati kwa kushirikiana na Oryx wameamua kutoa tuzo kwa Rais huku akitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!