Thursday , 4 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana washauriwa kupima VVU kukabilian ongezeko laa maambukizi
Habari Mchanganyiko

Vijana washauriwa kupima VVU kukabilian ongezeko laa maambukizi

Spread the love

 

MWAKILISHI wa Mtandao wa vijana wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania Cyprian Komba amewataka vijana kujitokeza kupima  Virusi vya UKIMWI ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi linalowakumba vijana. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).  

Kwa mujibu wa utafiti wa viashiria vya UKIMWI uliofanywa na Serikali mwaka 2022/23 watu 60,000 wamepata maambukizi ya VVU huku asilimia 40 ya maambukizi hayo ni kutoka kwenye kundi la vijana wa miaka 15-24.

Komba alisema hayo kwenye kongamano la vijana juu ya elimu ya masuala ya UKIMWI lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Chuo kikuu cha sokoine cha Kilimo (SUA) na Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) liilofanyika kwenye SUA kwa ufadhili wa USAID na Epics.

Alisema katika asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi hayo mwaka 2022/23 asilimia 80 ni vijana wa kike.

Komba alisema Serikali imehakikisha inaweka sehemu ya vijana kwenye kutoa maamuzi ili kueleza mapendekezo yao juu ya VVU na walipo sababu mwanzoni vijana hawakupewa nafasi.

Alisema takwimu za mwaka 2022 za utafiti wa DHIS zinasema bado uelewa wa vijana kwenye masuala ya VVU upo chini na kufanya Serikali kushirikiana na Asasi mbalimbali za kiraia kuwaelimisha kupitia makongamano ili wapime na kujua afya zao.

Naye mmoja wa wanafunzi wa SUA Nora Charles aliishukuru NACOPHA kwa kuwapatia elimu hiyo itakayowafanya kuzingatia afya zao kwa kupima kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kufikia malengo waliyokusudia.

“Tumeanza kupata uelewa kuwa tusipopima hatutotimiza ndoto zetu na kubaki na miili dhoofu ikiwa tuna maambukizi bila kujua na tukipima hata kama tukikutwa na maambukizi bado tunayonafasi ya kutimizia malengo yetu kwa kupata na kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARV)” Alisem.

Awali Mwakilishi wa TACAIDS Charles Hinju aliwaasa vijana kujiepusha na hali hatarishi za kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa kuacha kuiga Maisha ya wengine na kuzimudu hali za miili yao.

Alisema mtu anakuwa hatarini kupata maambukizi kutokana na kutofanyiwa tohara, unyanyasaji wa kijinsia, umaskini wa kipato unaopatikana kutokuwa na kuishiwa fedha za matumizi ‘boom’ na hivyo kutafuta wa kuwasaidia na kuangukia kwenye magonjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia, Nyusi wapongeza mkakati wa utanuzi PBZ, yakaribishwa kufungua tawi Msumbiji

Spread the loveRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Bwire Mtendaji mpya DAWASA

Spread the loveMhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia aahidi ushirikiano Rais mpya TEC

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waziri amtaka MNEC CCM Rukwa kuheshimu uamuzi wa Serikali kufunga Ziwa Tanganyika

Spread the loveNAIBU Waziri wa Mifugo na Uvivu, Alexander Mnyeti, amemtaka Mjumbe...

error: Content is protected !!