Thursday , 4 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Tofauti kati ya Rais Ruto, Naibu wake zaanikwa
Habari MchanganyikoKimataifa

Tofauti kati ya Rais Ruto, Naibu wake zaanikwa

Spread the love

TOFAUTI za kimtizamo kati ya Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua zimeendelea kuonekana wazi baada ya wawili kukinzana kuanzia  Jumapili tarehe 30 Juni 2024 kuhusu suala nyeti yanayohusu usalama wa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Katika mahojiano na wahariri wa mashirika makuu ya habari nchini Ikulu ya Nairobi juzi Jumapili usiku, Rais Ruto alikana madai ya Gachagua kwamba Shirika la Kitaifa la Ujasusi (NIS) lilifeli kutoa habari za kutosha kwake na vikosi vya usalama kabla maandamano ya vijana kupinga Muswada wa Fedha wa 2024.

Rigathi Gachagua

Dk. Ruto alisema kulikuwa na habari tosha za kijasusi kwamba wahalifu walikuwa wakipanga kuingilia maandamano ya amani ya Jumanne tarehe 25 Juni 2024.

“Hii ndio maana tulijiandaa kukabiliana na hali hiyo. Endapo hatungejiandaa tungekuwa tukitoa idadi tofauti ya waliokufa,” Dk. Ruto akasema.

“Wahalifu hao, walikuwa wamelenga kulemaza kabisa asasi muhimu za serikali. Hii ndio maana walipovamia majengo ya bunge walikwenda moja kwamba hadi stoo ya silaha na katika kaburi la Jomo Kenyatta,” akaongeza.

Baada ya maandamano hayo yaliyopelekea vifo vya idadi ya watu 39, Gachagua alielekeza lawama kwa Mkurugenzi Mkuu wa NIS, Noordin Haji kwa kile alichodai ni kufeli kutoa habari za kijasusi kwa Rais Ruto kuhusu maandamano ya kupinga mswada huo tata.

Akizungumza mjini Mombasa, Naibu Rais alimtaka Haji kujiuzulu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Haji anatakiwa kujiuzulu kwa kutomwarifu Rais hisia za Wakenya kuhusu Muswada wa Fedha na kunyamaza wakati wahalifu fulani walikuwa wakipanga kushambulia majengo muhimu ya serikali kama vile bunge. Amemuaibisha Rais na serikali na hivyo hana budi ila kujiuzulu,” Gachagua akasema.

Wakati huo huo, saa chache kabla ya Rais Ruto kufanya mahojiano na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi, Gachagua alikuwa katika kaunti ya Bomet akikiri kuwa kumekuwa na tofauti kati yake na bosi wake.

Hata hivyo, aliwahakikishia Wakenya kwamba watasuluhisha tofauti zao ili waendelee kusukuma gurudumu la kuliongoza taifa hili vizuri.

“Sina shaka kwamba Rais na mimi ni marafiki wa dhati na hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kuja katikati yetu. Tutasuluhisha masuala yote yaliyoibuka kati yetu. Tutatoa wito kwa viongozi kushusha joto la kisiasa,” Gachagua akasema.

Alikuwa akihutubia katika Kanisa la Deliverance mjini Kaplong, Bomet wakati wa ibada ya Jumapili na harambee ya kuchanga pesa kuendeleza kanisa hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Waingereza kuifuta historia ya Conservatives leo?

Spread the loveWaingereza milioni 50 wanatarajiwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu leo...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Biden agoma kujitoa uchaguzi Novemba, aangukia pua kura za maoni

Spread the loveRAIS wa Marekani, Joe Biden amekataa kujitoa kwenye uchaguzi wa...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia, Nyusi wapongeza mkakati wa utanuzi PBZ, yakaribishwa kufungua tawi Msumbiji

Spread the loveRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Bwire Mtendaji mpya DAWASA

Spread the loveMhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji...

error: Content is protected !!