Friday , 5 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania, Msumbiji kuanzisha kituo kimoja cha forodha
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania, Msumbiji kuanzisha kituo kimoja cha forodha

Spread the love

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema yeye pamoja na Rais wa Msumbiji, Philip Nyusi wamekubaliana kuanzisha sasa kituo kimoja cha forodha Mtambaswala kitakachohamasisha biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa Msumbiji, Philip Nyusi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema mwaka juzi 2022 biashara ya Tanzania na Mozambique ilikuwa Dola milioni 57.8 lakini mwaka jana tumeshuka.

“Kwa hiyo tumekubaliana kuangalia sababu gani, labda usalama ulizorota, baadhi ya mipaka vile vichochoro wanavyopita wafanyabiashara tulifunga. Inawezekana pia baadhi ya transaction hazipatikani official. Kama mnavyojua mpaka wetu ni mrefu. Kwa hiyo wafanyabishara wanapenya penya na zile takwimu zinatupita,” amesema.

Aidha, amesema kwa kuwa nchi zinazozalisha korosho kwa wingi Afrika zimekuwa zikitofautiana bei ya zao hilo katika soko la dunia, sasa wakuu wa nchi hizo wamekubaliana kuwa na umoja wao.

“Tunakwenda njia tofauti ambazo ni za kuwafanya watu wanaonunua korosho ndani angalau basi inone kidogo. Kwa hiyo tumekubaliana kuunda umoja, na mnakumbuka alipokuja Rais wa Guinea Bissau, Mheshimiwa Embalo nilimuuzia wazo hili naye amekubaliana. Kwa hiyo kwa pamoja sasa wazalishaji wa korosho Afrika utakwenda kufanya umoja wetu ili tuwe na sauti moja katika masoko,” amesema Rais.

Rais Nyusi ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu, anatarajiwa pia kuungana na Rais Samia kufungua rasmi maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama sabasaba kesho Jumatano jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

TCB yaja na huduma za ubunifu kidijitali maonesho Sabasaba

Spread the loveBenki ya Biashara Tanzania (TCB) ambayo ni moja ya taasisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Kampuni ya DL GROUP kulipa wafanyakazi ndani siku saba

Spread the loveMWEKEZAJI wa viwanda na mashamba ya chai yaliyopo mkoani Iringa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Shilole balozi mpya Oryx gesi kuhamasisha matumizi nishati safi

Spread the loveKAMPUNI ya Gesi ya Oryx imemtangaza Mama Lishe, Zuwena Mohamed...

ElimuHabari Mchanganyiko

NMB yazipiga tafu sekondari Dar kwa vifaa vya milioni 10

Spread the loveBenki ya NMB imekabidhi meza 90 na viti 90 vyenye...

error: Content is protected !!