Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kinara Afrika usambazaji umeme kwa wananchi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania kinara Afrika usambazaji umeme kwa wananchi

Spread the love

Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kusambazaji umeme kwa wananchi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitoa pongezi hizo  leo tarehe 4 Juni 2024 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Nathan Belete amesema kuwa benki hiyo inatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfumo mzuri wa kusambaza nishati kwa Watanzania.

“Hapa Afrika, Tanzania ni mfano mzuri katika usambazaji wa Nishati ya Umeme kwa wananchi. Tumejipanga kuwa na mazungumzo zaidi na kuona namna bora zaidi ya kusaidia katika masuala ya nishati safi ya kupikia kwa kufadhili na kuhusisha sekta binafsi kwa kuangalia fursa zilizopo,” amesema Belete.

Aidha, Belete amesema kuwa Benki hiyo inafadhili pia mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 ukutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Amesema kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuiendeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumzia pongezi hizo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameishukuru Benki ya Dunia kwa pongezi hizo na kusema kuwa Benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na kuwa wamekuwa na ajenda ya kushirikiana katika miradi ya nishati.

“Tumefurahi kusikia nchi yetu imepiga hatua na tumejipanga kuendeleza miradi mingine ya nishati ili kuhakikisha kuna utoshelevu wa Nishati hiyo nchini,” amesema Dk. Biteko.

Ameongeza “Tutaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia na Rais Samia amekuwa akisisitiza kila fedha tunayopata lazima iwe na thamani kwa wananchi. Wizara pamoja na Shirika letu la umeme TANESCO limepongezwa kwa kushughulikia vizuri suala la nishati nchini, hata hivyo ni lazima kuangalia mbali zaidi si tu kuridhika kwa hapa tulipofika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!