Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Tamasha la utamaduni na utalii Kanda ya Ziwa lazinduliwa Dar
Habari MchanganyikoMichezo

Tamasha la utamaduni na utalii Kanda ya Ziwa lazinduliwa Dar

Spread the love

 

TAMASHA kubwa la kimataifa la utamaduni na utalii linalojulikana kama Lake Zone Cultural and Tourism Festival limezinduliwa rasmi Jijini Dar es Salaam leo Juni 7, 2024 kwa lengo la kuwafikia washiriki wengi zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uzinduzi huu unakuja ukiwa umebaki mwezi mmoja tu kabla ya tamasha hilo la aina yake kufanyika huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Uzinduzi huo umefanywa na kampuni ya Kilimanjaro One Travel and Tours ambao ndio waandaaji wakuu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo Baraza la Sanaa Tanzania, Bodi ya Utalii Tanzania, wadau wa utaaduni kutoka Bariadi, Simiyu na waandishi wa habari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Travel and Tours Christina Emmanuel amesema, hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo ambayo inajihusisha na masuala ya utalii na utamaduni kuandaa tamasha hilo ambalo litakuwa na muitikio mkubwa kwa wakazi wa Simiyu na mikoa ya jirani.

“Tamasha hili linatarajiwa kufanyika mwezi wa saba na ninayo furaha kukufahamisha kuwa litafanyika kwa siku tatu mfulululizo Julai 5, 6 na kilele chake kitakua Julai 7 ambapo pamoja na mambo mengine tunategemea kuwa na maonyesho mbalimbali ya masuala ya utamaduni na utalii katika Uwanja wa Halmashauri na kuwavutia washiriki na watazamaji zaidi ya 7000 kwa siku hizo tatu,” alisema.

Aliongeza kuwa tamasha hilo litakuwa na vionjo mbalimbali ikiwemo ngoma inayohusisha makabila ya Wagika na Wagulu, maonyesho, michezo mbalimbali na vyakula ” ameongeza.

Nae, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mohamed Hatibu alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wafanyabiashara, makampuni, taasisi na mashirika kujitokeza na kuunga mkono kama njia moja wapo pia ya kuiunga mkono Serikali katika kuutangaza utamaduni na utalii wa Simiyu.

“Tumejiandaa vizuri na tuna uhakika tamasha hili litafanikiwa na litakuwa la kila mwaka,” alisema na kuongeza kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuwavutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa wa BASATA, Edward Buganga amewasifu waandaaji kwa kuandaa tamasha hilo katika kuendeleza utamaduni na Utalii hapa nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuliunga mkono tamasha hilo kwa hali na mali.

“Ni tamasha kubwa la aina yake ambalo sisi kama Watanzania tunapaswa kujivunia kuwa hili ni tamasha la kwetu kwa maendeleo ya utamaduni na utalii wetu,”alisema na kusisitiza kuwa Basata itatoa ushirikiano mkubwa kwa waandaaji ili tamasha hilo lifanyike kwa ufanisi mkubwa.

Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw.Nassor Garamatatu aliipongeza Kilimanjaro one Travel and Tours kwa kuona umuhimu wa kuunganisha utalii na utamaduni kwani haviwezi kutenganishwa.

“Sasa hivi sisi kama bodi tumejikita sana katika kutangaza utalii wa utamaduni ndio maana tuko tayari kuliunga tamasha hili mkono ili tutangaze utamadunina vivutio vya utalii kwa mkoa wa Simiyu.

Baadhi ya wabia na wadhamini wa tamasha hili ni pamojja na Tigo, NMB Bank, Z & M General Traders, Widescope Interprises Limited, na Carehealth and Hospitality Services.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!