MWENYEKITI mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu), ameanza kazi rasmi licha ya ushindi wake kuwekewa pingamizi na mtangulizi wake, Mchungaji Peter Msigwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X, jana Jumatano, Sugu ameandika ameongoza kikao cha kwanza cha uongozi wa Kanda hiyo.
“Leo nimeongeza kikao kazi cha kwanza Kanda ya Nyasa, viongozi wote wa juu wameshiriki yaani Makamu Mwenyekiti, Katibu na mtunza hazina pamoja na wenyeviti wa mabaraza ya Bazecha na Bavicha. Nyasa Moja,” ameandika Sugu.
Sugu ameanza kazi huku kukiwa na rufaa ya kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi wa kanda hiyo uliyofanyika hivi karibuni
Rufaa hiyo ilikatwa Jumapili iliyopita na Msigwa, ambaye alikuwa mshindani wa karibu na Sugu.
Katika Uchaguzi huo, Sugu aliyepata kura 54, alimshinda Msigwa kwa kura 2.
Msigwa amekata rufaa hiyo katika Kamati Kuu ya Chadema, akiomba matokeo hayo yafutwe Kisha uchaguzi ufanyine upya kwa madai kuwa wa awali haukuwa halali.
Leave a comment