SERIKALI ya Tanzania, imesema haijaweka rehani rasilimali za nchi ili kupata mkopo wa zaidi ya Sh. 6.7 trilioni, kutoka katika Serikali ya Korea Kusini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Ufafanuzi huo umetolewa leo tarehe 4 Juni 2024, jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, baada ya baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa kudai Tanzania imetoa sehemu ya bahari na madini kama dhamana ya kupata mkopo huo.
“Labda nideme kwamba Serikali yetu haijaweka rehani kitu chochote au mali yoyote kama ilivyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kinamii. Korea haijapewa sehemu ya bahari yetu mkopo huu haunaasharti yoyote ya kwueka rehani kitu chochote,” amesema Matinyi.
Matinyi amevitaka vyombo vya habari vilivyotoa madai hayo kuomba radhi akidai vimefanya upotoshaji.
“Tunatarajia waliopotosha watarekebisha na kuomba radhi wasomaji wao kwa kutoka taarifa zisizokamili au kwa kupotosha,” amesema Matinyi
Matinyi amesema mkopo huo ni wa masharti nafuu ambao utataolewa ndani ya miaka mitano. Utaanza kulipwa baada ya miaka 25 kwa muda wa miaka 40.
Leave a comment