Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kabla ya uteuzi huu Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imesema Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dk. Alphonce Biola Chandika ambaye amemaliza muda wake.
Leave a comment