MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa sasa ameacha ubabe na kuwataka viongozi wengine wa umma kuacha masuala ya ubabe. Anaripoti Faki Ubwa …(endelea).
Chalamila amebainisha hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu za mkoa mbele Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari.
“Tuendelee kuwa viongozi wazuri tutakaoepukana na masuala ya kibabe. Wakuu wa Wilaya waliokuwepo hapa simameni Rais awaone Bomboko wa Ubongo na Saad Mtambule wa Kinondoni. Mheshimiwa Rais Meseji yako tumeisikia ingawa mimi nimeshaacha,” amesema Chalamila.
Kauli hiyo ya Chalamila imekuja siku chache baada ya Rais Samia kukemea tena ubabe wa wakuu wa mikoa na wilaya kutokana na kutumia vibaya mamlaka yao ya kumuweka mtu mahabusu kwa saa 48.
Rais Samia alitoa kauli hiyo tarehe 15 Juni mwaka huu wakati akipokea Ripoti ya Kamati ya Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.
Leave a comment