Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Chalamila aonya wanafunzi elimu ya juu kuacha kulalamika
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chalamila aonya wanafunzi elimu ya juu kuacha kulalamika

Spread the love

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wanafunzi vyuo vikuu kuachana na utamaduni wa kulalamika, badala yake wawe mabalozi wazuri wa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pia ameiagiza Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu (HELSB) kuweka kambi katika chuo hicho ili kuwasaidia wanafunzi kufuata taratibu zote za kuomba mikopo bila kukosea ili unapokuja wakati wa kutolewa mikopo pasiwe na malalamiko ya mwanafunzi kukosa mkopo.

Chalamila ametia maagizo hayo jana Alhamisi alipofanya ziara katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika vyuo vikuu vya Mkoa huo.

Chalamila pia alipata wasaa wa kuzungumza na menejimenti ya chuo hicho na baadae kukutana na wanafunzi katika ukumbi wa mikutano.

“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa uwekezaji mkubwa katika nyanja za elimu katika chuo hiki tayari ameshatoa pesa si chini ya bilioni 19, kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu ya chuo hicho” alisema RC Chalamila.

Aidha, RC Chalamila amesema kwa upande wa mikopo ya vyuo vikuu Rais Samia ameongeza fedha katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa ajili ya kutanua wigo wa wanufaika wa mikopo, hivyo   wanafunzi watumie vizuri fursa hiyo.

Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo, Prof Stephen Maluka Serikali ya Rais Samia tayari imeshatoa kiasi cha pesa sio chini ya  bilioni 19 ambazo zinakwenda kujenga majengo mawili ya kisasa ya ghorofa 5, viwanja vya kisasa vya michezo hususani kwa wenye uhitaji, sweeming pool, na ukarabati wa Hosteli pale Mbagala pamoja na Internet ambayo tayari imeshawekwa katika maktaba chuoni hapo.

Chalamila aliambatana na wataalam na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na chama wakiwemo  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, wataalam kutoka NHIF, NACTVET,  TCU, NIDA pamoja na Bodi ya Mikopo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!